Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?
Supplementary Question 1
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri yaliyotolewa na Serikali, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza. Kwa kuwa Kata ya Ipunga na Kata ya Isalalo Serikali imedai kwamba bado hazijanufaika na upatikanaji wa huduma za simu za uhakika. Ni lini sasa utafiti huo utakamilika ili wananchi wale ambao wamesubiri kwa muda mrefu waweze kunufaika na mawasiliano ya simu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Pamoja na kwamba Kata ya Nyimbili mmejenga minara miwili ambayo kwa kweli ninaipongeza Serikali, lakini yapo maeneo kutokana na jiografia ya Kata ya Nyimbili yapo bondeni na mengine yapo, kuna milima mingi, hakuna mawasiliano ya simu kwa uhakika katika maeneo kama Hantesya, maeneo kama Shititi, Nyanyi na Namwangwa yote hayapati mawasiliano. Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanafikiwa vizuri na mawasiliano yanapatikana kwa wakati? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nipokee shukurani za Mheshimiwa Japhet Hasunga na wewe pia nikupongeze kwa ufuatiliaji mzuri na nikuhakikishie tu kwamba huu utafiti tutahakikisha unafanyika katika mwaka huu wa fedha ili mwaka ujao wa fedha kadri pesa inavyopatikana mapema sana wananchi hawa waweze kupelekewa huduma ya mawasiliano kwa sababu ndiyo hamu ya Mheshimiwa Rais wetu kuona kwamba vijiji vyote vinafikiwa kupata mawasiliano ya uhakika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali katika mazingira haya yenye miinuko tayari wataalamu wetu wanaendelea kufanyia kazi, kama ni ku-upgrade na kuona kwamba signals ziwe za mfumo mzuri labda wa 3G watafanya, lakini maeneo ambayo haiwezekani, basi minara mipya itapelekwa, na tayari tuna ongezeko la bunch ya minara zaidi ya 200, TTCL pia watakwenda kwenye maeneo haya yote ambayo siyo rafiki wa biashara lakini wananchi wetu ambao Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anawahudumia wataweza kufikiwa. (Makofi)
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?
Supplementary Question 2
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona. Jimbo la Karagwe, Kata ya Bweranyange, Kijiji cha Muguruka hakuna mawasiliano kabisa. Ningependa kujua ni lini Serikali itapeleka mawasiliano katika Kijiji hicho? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na maeneo haya ya Karagwe. Kadri fedha inavyopatikana, tutahakikisha maeneo haya yote uliyoyataja tutaweza kuyafikia. Nashukuru sana. (Makofi)
Name
Neema William Mgaya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?
Supplementary Question 3
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika Mkoa wa Njombe, Jimbo la Makambako, Kata ya Lyamkena maeneo ya Kiumba Kati, Makatani na Muungano, lini Serikali itajenga minara ili sehemu hii iweze kupatiawa mawasiliano, maana mawasiliano hakuna kabisa? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo haya ya Njombe, Makambako Kata zote alizozitaja Mheshimiwa Neema, tayari Mheshimiwa Jerry, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, amewaagiza Wataalam, wameenda huko, wanaendelea kufanya tafiti na tafiti zitakapokamilika, Kata hizi zote zitakuwa wanufaika. Hivyo, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge katika ufuatiliaji huu, ahsante. (Makofi)
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.
Kata ya Maroroni katika Kijiji cha Samaria na Kata ya Uwiro, Kisimiri Juu kuna changamoto kubwa sana ya mawasiliano ya simu. Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga minara ya mawasiliano katika maeneo hayo? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kijiji cha Samaria na Kijiji hiki jirani ambavyo amevitaja Mheshimiwa Dkt. Pallangyo, nimhakikishie kwamba mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunavifikia hivi vijiji vyote na kujenga minara ya mawasiliano na wananchi wote waweze kunufaika na hali nzuri ya mawasiliano, ahsante. (Makofi)
Name
Aziza Sleyum Ally
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?
Supplementary Question 5
MHE. AZIZA S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa upo utapeli mkubwa ambao wanafanyiwa wananchi kupitia minara hii na kuwalaghai kuwa watakapotoa pesa watawekewa minara na watu hao ni matapeli, je, Serikali ina kauli gani ya kuwaelimisha wananchi ili wasizidi kutapeliwa na wananchi hao? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie Bunge lako Tukufu kuwaambia wananchi wote wa Tanzania kwamba, ujenzi wa minara unafanywa na wataalam ambao wapo, wana vibali kamili kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Naomba wale wote ambao wanafika huko, huwa wanaongozana na Watendaji wetu, wataweza kuonesha vitambulisho, lakini vilevile wawatumie ninyi Waheshimiwa Wabunge kuhakiki kama kweli hao waliokwenda ni wataalamu waliopata vibali kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. (Makofi)
Name
Amandus Julius Chinguile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nachingwea
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?
Supplementary Question 6
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kata za Kilimarondo, Kipara Mtua, Mtua na Stesheni maeneo ya Mchangani hali ya mawasiliano ni ngumu. Je, ni lini Serikali itajenga minara kwenye Kata hizi? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kwamba kata hizi alizozitaja naomba tu nimtoe hofu kwamba kadri fedha inavyopatikana mwaka ujao wa fedha 2025/2026 tutahakikisha maeneo haya na yenyewe tunayafikia na minara inajengwa na wananchi wanakwenda kunufaika na hali nzuri ya mawasiliano ya Tanzania. (Makofi)
Name
Innocent Sebba Bilakwate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali wa kujenga minara ya simu kwenye Kata ya Ipunga, Nyimbili na Isalalo ili kuboresha mawasiliano?
Supplementary Question 7
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Makao Makuu ya Wilaya ya Kyerwa kuna shida kubwa ya mtandao na shughuli nyingi zinashindwa kufanyika. Je, ni lini Serikali itaboresha mtandao pale uweze kufanya kazi vizuri? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Makao Makuu ya Kyerwa, kwa sababu ni Makao Makuu, ninaamini minara ipo. Kwa hiyo, tutakachokifanya ni kuwatuma watoa huduma ambao tayari wanafanya huduma pale, wakaboreshe kama ni ku-upgrade kutoka 2G, 3G, 4G ili iweze kupatikana mawasiliano ya uhakika. (Makofi)