Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 298 2025-05-13

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: -

Je, lini ujenzi wa kivuko cha abiria kutoka Kakukuru kwenda Gana – Ukerewe kitaanza kujengwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia wakala wa ufundi na umeme TEMESA katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 inaendelea na utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa vivuko mbalimbali nchini. Aidha, baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa daraja la JPM, yaani pale Kigongo Busisi Mkoani Mwanza, vivuko vinavyotoa huduma katika eneo hilo vitagawanywa katika maeneo yenye uhitaji wa vivuko katika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni pamoja na Kakukuru, kwenda Gana Wilayani Ukerewe. (Makofi)