Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kivuko cha abiria kutoka Kakukuru kwenda Gana – Ukerewe kitaanza kujengwa?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Serikali na nina maswali mawili ya nyongeza. Naipongeza Serikali kwa mpango huo na ninatambua kuna vivuko vingine vinafanyiwa maboresho kama kivuko cha MV Nyerere na kadhalika. Vivuko hivi vikishakamilika au vikihamishiwa Ukerewe kunatakiwa kuwe na magati ambayo yatasaidia vivuko hivi kutua, lakini sioni dalili zozote za maandalizi ya magati kwenye eneo la Gana, Kakukuru, Lutale wala Ilugwa. Ni nini mkakati wa Serikali kuanza maandalizi ya magati kwenye maeneo haya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwenye bajeti ya mwaka 2024 tulitenga pesa kwa ajili ya kujenga mabanda ya abiria kusubiri kwenye eneo la Bugolola, Bwisya pamoja na Bukimwi lakini sioni kazi yoyote inayoendelea. Ni nini mpango wa Serikali kujenga mabanda haya ya abiria kusubiri?

Name

Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia masuala haya ya vivuko na hasa katika Jimbo lake la Ukerewe ambalo linaunganisha sehemu kubwa na vivuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu magati, eneo hili ambalo nalisema ni sehemu ambayo kivuko kipya kinakwenda. Kwa hiyo, tunachofanya sasa hivi, ni usanifu ili kujenga magati ambayo yatahudumia katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vivuko vyote ambavyo vinafanya kazi, na tunajenga vivuko vipya, Mheshimiwa Mbunge atakubaliana nami kwamba tayari magati yanaendelea kujengwa na yapo kwenye hatua za mwisho kabisa. Kwa hiyo, sasa hivi tunachofanya katika maeneo haya ambayo ni mapya, sasa hivi tupo kwenye usanifu ili tuweze kuanza kujenga magati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, katika swali lake la pili kuhusu mabanda, tumetenga bajeti katika mwaka huu 2025, wakati tunaendelea na ujenzi wa vivuko vipya. Pia tuna mpango wa kujenga mabanda, na kazi hii Wizara imeipa TBA ambao wapo mwishoni kabisa kukamilisha usanifu wa mabanda kwa sababu haya mabanda hayafanani kati ya kituo na kituo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mpango huo upo na tupo hatua za mwisho za usanifu na baada ya hapo tutaanza ujenzi pia wa mabanda ili kutoa huduma katika maeneo hayo ya vivuko. Ahsante. (Makofi)

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kivuko cha abiria kutoka Kakukuru kwenda Gana – Ukerewe kitaanza kujengwa?

Supplementary Question 2

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mkoa wa Kagera baada ya kuona mafanikio ya ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi, tumeomba Wizarani kwamba, baadhi ya vivuko vipelekwe Magarini ili kutoa huduma sehemu za Ikuza na Mazinga. Pia kivuko kingine kipelekwe Rubafu ili kuunganisha Tanzania na Uganda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Waziri katika hivyo vivuko, ni vingapi ameainisha kwamba vitapelekwa kwenye maeneo hayo mawili ambayo yana uhitaji wa vivuko?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, vivuko vilivyokuwa vinatoa huduma pale Kigongo - Busisi ndiyo vivuko vikubwa katika Ziwa Victoria na vitakapopelekwa kwenye maeneo, maana yake, kama kulikuwa na vivuko viwili, vitahamishiwa kwenye maeneo mengine kwa sababu tulikuwa na vivuko vikubwa vitatu pale Misungwi, Sengerema na MV. Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama kuna kivuko kilikuwa na vivuko vitatu, maana yake vitagawanywa kwenda kwenye hatua tatu. Tunachokifanya sasa hivi ni tathmini ikiwa ni pamoja na mawazo ya Mheshimiwa Mwijage, kama kutakuwa na kivuko kikubwa, hivyo chenye sifa ya kuunganisha sisi na Uganda, basi tutafanya hivyo.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kivuko cha abiria kutoka Kakukuru kwenda Gana – Ukerewe kitaanza kujengwa?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumwuliza Mheshimiwa Waziri, kivuko cha MV Ilemela kilitengenezwa kwa ajili yaku-save kisiwa cha Base pamoja na Kayenze, lakini kutokana na uhitaji, kivuko kile kilianza kufanya kazi katika Kisiwa cha Bukimwi na kwa sasa mahitaji yamekuwa ni makubwa kiasi kwamba kivuko kile kimezidiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni ipo haja, aidha, kuweka vivuko viwili viwe vinapishana au kuongeza root ili kuweza kuondoa adha inayopatikana sasa, maana kuna magari yanaachwa, watu wanaachwa kwa sababu kivuko kimezidiwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Mbunge wa Ilemela kuhusu swali lake. Nataka nimhakikishie kwamba, bahati nzuri nilishatembelea eneo hilo la Kayenze ambapo hicho kivuko kinaanza, na tunapokuwa tunaboresha vivuko imeonekana kwamba idadi ya watu inaongezeka sana kwenye vivuko. Ndiyo maana pamoja na kukamilika kwa daraja la Kigongo - Busisi tutaongeza hivyo vivuko kwenda kwenye sehemu nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge kwamba, katika Awamu hii ya Sita tunajenga vivuko vitano vipya kabisa katika Ziwa Victoria ambapo tupo kwenye zaidi ya 85% kwenda 90.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hivyo vivuko vipya pia vitakapokamilika vitatoa nafasi ya vivuko vidogo kwenda kuhudumia kwenye sehemu nyingine. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, pia tutafanya study ambayo tunaendelea kuifanya kwa sababu tumeona watu wanaongezeka, magari yanabaki, tuone ama kuongeza kivuko kikubwa ama kuongeza kituo kuwa cha pili ili viwe vinapishana katika eneo hilo.

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kivuko cha abiria kutoka Kakukuru kwenda Gana – Ukerewe kitaanza kujengwa?

Supplementary Question 4


MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kisiwa cha Nafuba katika Jimbo la Mwibara ni mojawapo ya sekta kubwa sana ya biashara ya samaki jimboni. Je, ni lini Serikali itajenga kivuko cha kwenda Nafuba kutoka Nasimo?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRII WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe tu maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA, kwa sababu kazi yao ni kufanya tathmini na kufanya utafiti, aende akafanye utafiti na kuona kivuko kipi kitafaa na wapi kivuko kinaweza kujengwa ili kutoa huduma hiyo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameiomba.

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kivuko cha abiria kutoka Kakukuru kwenda Gana – Ukerewe kitaanza kujengwa?

Supplementary Question 5

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, wananchi wa Kata za Kwagunda, Mnyuzi na Hari wanashindwa kuvuka kutokea Korogwe kwa sababu ya daraja ambalo limekatika kwa muda sasa. Ni upi mpango wa Serikali juu ya daraja hili la Urengera ambalo limekatika zaidi ya mwaka mmoja?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mnzava kwamba, ni kweli kwamba vivuko tunavichukulia kama ni daraja ambalo linatembea. Kwa hiyo, alichouliza ni daraja, japo tunaongelea vivuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, daraja lile lilikatika katika kipindi hiki na Wizara imelichukulia kama ni dharura. Mheshimiwa Waziri alishatoa maelekezo, na hivi tunavyoongea, sasa hivi tupo kwenye hatua za mwisho kupata mkandarasi ili aweze kulijenga pia kwa udharura wake kama ilivyotokea kwa hilo daraja la Mheshimiwa Mnzava.