Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Finance and Planning Wizara ya Fedha 299 2025-05-13

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question


MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: -

Je, Serikali imewezesha miradi mingapi kwa utaratibu wa ubia wa Serikali na Sekta Binafsi?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 10A cha Sheria ya PPP Sura Na.103 kilianzisha Mfuko wa Uwezeshaji Ubia kwa lengo la kuziwezesha Mamlaka za Serikali kuandaa na kutekeleza miradi ya PPP. Aidha, Kifungu cha 5(1) cha Sheria hiyo imekipa Kituo cha Ubia (PPP Centre) jukumu la kutoa usaidizi wa kiufundi kwa Mamlaka za Serikali na Sekta Binafsi wakati wa uibuaji, maandalizi na utekelezaji wa miradi ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Hadi Aprili, 2025 jumla ya miradi 80 imewezeshwa na Serikali, na ipo katika hatua mbalimbali kama ifuatavyo: -

(i) Miradi mitatu ipo katika hatua ya utekelezaji;
(ii) Miradi minne ipo katika hatua ya majadiliano;
(iii) Miradi miwili ipo katika hatua ya ununuzi;
(iv) Miradi 26 ipo katika hatua ya upembuzi yakinifu;
(v) Miradi 13 ipo katika hatua ya upembuzi yakinifu wa awali; na
(vi) Miradi 32 ipo katika hatua ya andiko dhana.