Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, Serikali imewezesha miradi mingapi kwa utaratibu wa ubia wa Serikali na Sekta Binafsi?
Supplementary Question 1
MHE. ORAN M. NJENZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali, na kwa kuwa kuna miradi mingi ya maendeleo yenye mvuto wa kutekelezwa na uwekezaji wa sekta binafsi kwa njia ya PPP; na kwa kuwa sheria ya bajeti kifungu 7(3) kinaelekeza Serikali kutotenga bajeti kwenye miradi ambayo ina mvuto wa PPP, swali namba moja: Je, imejipanga vipi Serikali kutekeleza miradi ya barabara yenye mvuto na sekta binafsi ikiwemo barabara ya Igawa, Mbeya, Tunduma pamoja na bypass ya Uyole Songwe?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Je, Serikali imejipanga vipi kuhamasisha sekta binafsi kuingia ubia ili iweze kutekeleza ujenzi mpya na uboreshaji wa reli ya TAZARA ikiwemo na uendeshaji?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Njeza kwa namna anavyofuatilia katika suala zima la uwekezaji kwa utaratibu wa PPP. Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi na kuwaita kabisa kuandaa miradi tofauti tofauti kwa lengo la kushiriki katika miradi ya PPP na miradi yao ikionekana inafaa katika utaratibu huo, basi inafanyiwa kazi na hatimaye kufika kuweka saini na utekelezaji wa miradi tofauti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kipande cha Igawa alichokitaja Mheshimiwa Njenza, Igawa – Tunduma kwa sasa yupo mshiriki wa sekta binafsi ambaye anaandaa mradi kwa kupitia utaratibu wa PPP.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, Serikali ya Tanzania na Zambia zipo kwenye majadiliano kati yake na Serikali ya China, na kwa sasa imefika hatua nzuri, wakati wowote Serikali ya Zambia na Tanzania pamoja na Serikali ya China zitaweka saini kupitia kampuni ya CECC, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved