Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 23 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 300 | 2025-05-13 |
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARYAM AZAN MWINYI K.n.y. MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kuwawezesha wavuvi wa Kigamboni kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya uvuvi?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatekeleza mradi wa kuwawezesha wananchi kupitia dirisha la ECF/IMF kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) tangu mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo kwa awamu ya kwanza jumla ya boti 160 zenye thamani ya shilingi bilioni 11.5 zilitolewa kwa wanufaika 3,163.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya hao, idadi ya wanawake ni 1,008, na wanaume 2,155, ambapo, Kikundi cha Bright Fisheries chenye wananchi saba kutoka Kigamboni kilinufaika kwa kupatiwa boti ya kisasa ya uvuvi yenye ukubwa wa mita 14 na vifaa vyake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango wa bajeti wa mwaka 2025/2026, Wizara imetenga kiasi cha shilingi bilioni 9.5 kwa ajili ya kuendelea kuwezesha wavuvi kupata boti na vifaa bora vya uvuvi kwa mkopo wenye masharti nafuu wakiwemo wananchi wa Kigamboni. Aidha, utoaji wa boti hizo ni endelevu, hivyo Wizara inahamasisha wavuvi na vikundi vya wavuvi kuendelea kuomba mikopo hiyo ili waweze kunufaika na fursa hiyo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved