Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI K.n.y. MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuwawezesha wavuvi wa Kigamboni kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya uvuvi?

Supplementary Question 1

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza, je, ni lini Serikali itapeleka boti kwenye Ziwa Nyasa?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ziwa Nyasa tayari Serikali imeshapeleka boti. Kuna vikundi viwili ambavyo viliomba boti na jumla ya boti tano tumeshapeleka katika Ziwa Nyasa, lakini tunaendelea kupokea maombi, tupo tayari kuendelea kuongeza boti katika eneo hilo la Ziwa Nyasa.