Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 301 2025-05-13

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question


MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kujumuisha Mada ya ukatili wa kijinsia kwenye Masomo kuanzia Shule za Msingi nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya maboresho ya mitaala katika ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu mwaka 2023 ili kuhakikisha kuwa mitaala yetu inaendana na Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mitaala iliyoboreshwa, ukatili wa kijinsia pamoja na masuala mengine mtambuka yamechopekwa katika masomo mbalimbali katika ngazi zote za elimu. Aidha, somo jipya la Historia ya Tanzania na Maadili ambalo ni somo la lazima kwa wanafunzi wote kuanzia elimu ya Awali mpaka Kidato cha Sita lina mada mahususi zinazolenga kujenga umahiri wa mwanafunzi katika kuelewa na kupinga ukatili wa kijinsia.