Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kujumuisha Mada ya ukatili wa kijinsia kwenye Masomo kuanzia Shule za Msingi nchini?

Supplementary Question 1

MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali kwa mpango mzuri wa kuboresha mitaala ya elimu. Nauliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu juu ya suala zima la kuwajengea uelewa juu ya ukatili wa kijinsia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Serikali inahakikishaje kushirikiana na Wizara mbalimbali juu ya kutoa elimu juu ya suala zima la ukatili wa kijinsia?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la elimu Wizara na Serikali kwa ujumla tumeendelea kutoa elimu kwa jamii pamoja na wanafunzi kwa ujumla. Naomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kupitia Taasisi yetu ya Elimu Tanzania (TET) imeanzisha kituo maalum kabisa cha TV kinachohusiana na masuala ya kutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla katika maeneo hasa hasa ya masuala ya mitaala yetu kwa maana ya shule katika masomo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile TV hii imetusaidia kufundisha zile stadi za maisha na stadi za kazi, lakini sambamba na hilo imekuwa ni TV ambayo inawezesha kutoa hii elimu ya ukatili wa kijinsia kwa namna moja au nyingine. Kwa hiyo, elimu hii inaendelea, lakini ipo katika vituo vyote vya televisheni kwa kadri unavyopata muda, basi elimu hii imekuwa ikitolewa kwa jamii kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili kuhusiana na suala la kushirikiana ama mashirikiano na sekta nyingine au Wizara nyingine, ni kweli suala hili ni suala mtambuka. Kwa hiyo, sisi Wizara ya Elimu tukishirikiana na wenzetu wa TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, na Wizara ya Mambo ya Ndani tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwamba elimu hii inawafikia Watanzania wote au jamii yote kwa ujumla na hasa kwa kuanzisha madawati mbalimbali katika maeneo tofauti tofauti ambayo hususan yanahusika na masuala ya ukatili wa kijinsia. Nakushukuru sana.