Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Water and Irrigation Wizara ya Maji 302 2025-05-13

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question


MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kusambaza maji Kata za Kaboha, Shabaka, Nyang’hwale, Nyaburanda, Mwingiro, Nyugwa ili kuondoa shida ya maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ya maji katika Wilaya ya Nyang’hwale inapatikana kwa baadhi ya maeneo ya Kata za Kaboha, Shabaka, Nyang’hwale, Nyaburanda, Mwingiro pamoja na Nyugwa kupitia visima virefu tisa, visima vya pampu za mkono saba pamoja na mtandano wa bomba. Katika kutatua changamoto hiyo, Serikali inaendelea na mpango wa muda mfupi wa kuchimba visima na kujenga miundombinu rahisi ya kutolea huduma katika baadhi ya vijiji vya kata hizo kupitia programu mbalimbali ikiwemo Programu Maalum ya Uchimbaji wa Visima 900.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utafutaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango wa muda mrefu wa miradi mikubwa ya kimkakati inayohusisha Upanuzi wa Mradi wa Maji (JWPP) kwenda vijiji vyote vya Kata ya Kaboha, pamoja na Upanuzi wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Nyijundu kwenda Nyang’hwale.