Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 23 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 303 2025-05-13

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwagawia Wananchi sehemu ya eneo la Pori la Kigosi ili litumike kwa shughuli za kiuchumi?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Misitu Sura Na. 323, inaruhusu baadhi ya shughuli za kiuchumi kufanyika kwenye maeneo ya hifadhi za misitu kwa kuzingatia mahitaji ya uhifadhi. Aidha, Serikali imetoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli za kiuchumi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na ufugaji wa nyuki, uchimbaji wa madini, uvuvi, utalii wa aina mbalimbali, utafiti na mafunzo ambapo hadi sasa wafugaji nyuki wapatao 3,061 kutoka katika vijiji 105 wamepewa vibali vya kuingia ndani ya hifadhi na wameweza kutundika mizinga ya nyuki ipatayo 585,713.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Serikali kupitia Wizara ya Madini inaendelea na uratibu wa kutoa vibali kwa shughuli za madini kwa kuzingatia tafiti za madini ambapo kazi hiyo inafanyika kwa kuzingatia uhifadhi kwa mujibu wa Sheria za Misitu, Madini na Mazingira.