Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwagawia Wananchi sehemu ya eneo la Pori la Kigosi ili litumike kwa shughuli za kiuchumi?

Supplementary Question 1

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na pia nashukuru kwa majibu ya Serikali. Nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Iponya, Kijiji cha Sango; Kata ya Isebya, Kijiji cha Nyashinge; na Kata ya Ilolwangulu, Kijiji cha Kanangwe; nimeyataja haya maeneo, je, yuko tayari kutuma timu ya Wizara yake ije iangalie ili ione kama yanaruhusiwa ili wananchi waendelee kufanya shughuli? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Wilaya ya Mbogwe pamoja na wilaya ya jirani, sisi kule bado tunatumia kuni na wananchi huwa tunawapa semina kulingana na vibali kama alivyosema ikiwemo kukata mkaa lakini kumekuwa na askari ambao sio waaminifu sana, wakimwona mtu tu na mkaa wanamkimbiza, wanamfanyia fujo na kumuumiza. Je, ni maelekezo gani anayatoa kama Waziri mwenye Wizara? (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iko tayari kutuma timu kwenda kushirikiana na uongozi wa wilaya katika maeneo haya ili kufanya hiyo tathmini na baadaye tutaleta majibu kwa Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la pili, uchomaji wa mkaa una taratibu na sheria ambazo unazingatiwa. Natoa maelekezo kwa wahifadhi wetu katika maeneo yote nchini kuzingatia sheria na taratibu zinavyotaka katika kusimamia jambo hili. (Makofi)