Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 5 Sitting 4 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 47 2016-11-04

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. COSTANTINE J. KANYASU aliuliza:-
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kupitia mtandao wa Twitter alitangaza kuzuia timu yoyote katika kundi ā€žCā€Ÿ la Ligi Daraja la Kwanza kupanda daraja kabla ya mechi zao kukamilika na kabla ya vikao halali vya uchaguzi kufanyika:-
Je, Serikali haioni kwamba, maamuzi yalifanywa kinadharia na uonevu mkubwa kwa Timu ya Geita Gold Sport?

Name

Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Costantine John Kanyasu, Mbunge wa Geita Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, maamuzi yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) dhidi ya Timu ya Geita Gold Sports ya kuishusha Daraja kutoka la Kwanza kwenda la Pili hayakuwa ya kinadharia au uonevu. Yalizingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kushughulikia malalamiko yanayotokana na mwenendo wa mashindano husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa TFF baada ya kupata malalamiko kutoka timu za Kundi ā€žCā€Ÿ kuhusu timu ya Geita Gold Sports kukiuka Kanuni za Mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza kwa kujitangazia kuwa ni washindi katika kundi hilo hata kabla haijakamilisha kucheza mechi moja, iliielekeza Kamati ya Nidhamu kufanya uchunguzi wa suala hilo na kuchukua hatua stahiki. Kupitia vikao vya maamuzi vilivyokaa kujadili suala hilo ilionekana kuwa, timu ya Geita Gold Sports imekiuka Kanuni za Ligi na hivyo ilistahili kupewa adhabu ya kushushwa kutoka Daraja la Kwanza hadi la Pili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wa TFF anao utaratibu wa kuvitahadharisha vilabu vinavyoshiriki mashindano ya ligi katika ngazi mbalimbali kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima hivyo, taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wa twitter ilikuwa ni sehemu ya tahadhari hiyo. Aidha, napenda kuchukua fursa hii kuvitaka Vyama vya Michezo, Mashirikisho, Vilabu na wadau kwa ujumla kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa katika kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango, maamuzi, chaguzi mbalimbali kwa maslahi ya vyombo hivyo na Taifa kwa ujumla.