Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 18 Sitting 4 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 41 2020-01-31

Name

Maulid Said Abdallah Mtulia

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

MHE. MAULID S. MTULIA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuimarisha Sekta ya Michezo kwa kuandaa Wakufunzi wa Michezo, kujenga viwanja vya kisasa na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya michezo?

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maulid Said Mtulia, Mbunge wa Kinondoni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha Sekta ya Michezo, Serikali imeendelea kutoa mafunzo ya aina mbalimbali yanayohusu taaluma tofauti za Michezo. Kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, elimu ya michezo hutolewa katika ngazi ya Shahada kupitia idara ya maalum ya Physical Education and Sports Science. Aidha, kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Mkoani Mwanza, Serikali inaendelea kutoa mafunzo ya utawala katika Michezo pamoja na ukufunzi katika michezo mbalimbali katika ngazi ya Stashahada, Diploma in Sport Admistration and Coaching ambayo hutolewa kwa muda wa miaka miwili.

Mheshimiwa Spika, suala la ujenzi wa miundombinu siyo la Wizara peke yake, letu sote ikiwemo sekta binafsi na halmashauri zote nchini.