Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2015-2020 | Session 15 | Sitting 31 | Energy and Minerals | Wizara ya Nishati | 261 | 2019-05-20 |
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza:-
Je, Megawati moja ya umeme inazalishwa kwa bei gani na inauzwa kwa bei gani (unit cost)?
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA (K.n.y. WAZIRI WA NISHATI) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Shirika la Umeme Nchini, inagharamia uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme hadi kwa mteja kwa kuweka miundombinu husika ya umeme. Kwa sasa gharama ya kuzalisha uniti moja (Kwh) ya umeme kwa kutumia chanzo cha maji ni shilingi 36 na gharama ya kuzalisha uniti moja ya umeme kwa kutumia gesi asilia ni wastani wa shilingi 150. Gharama ya kuzalisha uniti moja kwa mitambo inayotumia mafuta ya dizeli katika maeneo yaliyopo nje ya Gridi ya Taifa ni shilingi 720 kwa uniti moja yaani Kwh moja.
Mheshimiwa Spika, bei ya kuuza umeme inatokana pia na gharama za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme. Kwa sasa bei ya kuuza umeme ni wastani wa shilingi 242 kwa uniti yaani Kwh.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved