Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 2 | Sitting 6 | Public Service Management | Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) | 77 | 2021-02-09 |
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. SAASISHA E. MAFUWE Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi aliyotoa Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni ya kuongeza watumishi 403 wa afya?
Name
Deogratius John Ndejembi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chamwino
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Saasisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha miaka ya 2015 hadi 2020, Serikali imeajiri jumla ya watumishi 14,479 wa kada mbalimbali za afya. Katika Mwaka wa Fedha 2020/ 2021 Serikali inatarajia kuanza kuajiri watumishi 75 wa kada mbalimbali za afya kwenye Wilaya ya Hai kwa ajili ya hospitali ya wilaya moja, vituo vya afya sita na zahanati 28 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved