Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 3 | Sitting 27 | Energy and Minerals | Wizara ya Nishati | 231 | 2021-05-11 |
Name
Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Longido
Primary Question
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA aliuliza:-
Umeme wa msongo mkubwa wa KV 400 toka Singida hadi Namanga umepita katika baadhi ya maeneo ya wazi na malisho ya mifugo 6 kwenye Vijiji vya Engikaret, Ranchi, Orbomba, Kimokouwa na Eorendeke; na fedha za fidia ilipendekezwa zitolewe kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ya Vijiji husika pamoja na watu binafsi ambao umeme huo umepita kwenye makazi yao:-
Je, ni lini fedha hizo zitatolewa?
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Steven Lemomo Kiruswa, Mbunge wa Longido, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Shirika la TANESCO inaendelea kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Singida hadi Namanga. Lengo kuu la mradi huu ni kuimarisha umeme katika Gridi ya Taifa na kuunganisha Tanzania na nchi za Zambia na Kenya katika gridi ya umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mradi huu mwezi Septemba, 2020 Serikali kupitia TANESCO ililipa fidia jumla ya shilingi bilioni 11.33 kwa wananchi wapatao 645 katika Wilaya ya Longido ikiwamo Vijiji vya Engikaret, Ranchi, Orbomba, Kimokouwa na Eorendeke. Malipo hayo yamelipwa kama ifuatavyo; Kijiji cha Eorendeke jumla ya shilingi 439,780,320, Kijiji cha Kimokouwa jumla ya shilingi 165,564,000, Kijiji cha Orbomba jumla ya shilingi 343,662,080 na Kijiji cha ranchi jumla ya shilingi 720,754,200.
Mheshimiwa Spika, malipo ya fedha hizi yalifanyika kwa njia ya hundi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved