Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 6 | Sitting 10 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 119 | 2022-02-14 |
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali italirejesha Shamba la kupumzishia Mifugo la Kinyangiri kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Francis Isack Mtinga, Mbunge wa Iramba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia umuhimu wa maeneo haya katika biashara ya mifugo na mazao yake, hususan kipindi hiki ambapo soko la nyama limezidi kuongezeka nje ya nchi, Serikali inakusudia kuendelea kuboresha maeneo yake yote ya mifugo ikiwa ni pamoja na eneo la Kinyangili ili kusudi biashara ya mifugo na biashara ya nyama nchini iweze kushamiri kwa kuzingatia viwango vyote vinavyotakiwa katika Soko la Kitaifa na Kimataifa. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved