Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali italirejesha Shamba la kupumzishia Mifugo la Kinyangiri kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama?
Supplementary Question 1
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja tu la nyongeza: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mpaka sasa Halmashauri ya Mkalama ndio wanaotunza shamba hili; na kwa kuwa, hatuna ugomvi na Wizara na tunajali sana maslahi ya umma: Je, Wizara ipo tayari sasa kukaa meza moja na Halmashauri ya Mkalama ili tuweze kukaa na kujadili matumizi bora zaidi ya eneo hili kuliko kuendelea kuwa shambapori kama ambavyo lilivyo sasa? Ahsante.
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Isack Francis Mtinga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, milango ya Wizara iko wazi. Tunawakaribisha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, wakiongozwa na Mheshimiwa Mbunge makini, waweze kuja tukae mezani kuzungumza na kuona hatima njema ya eneo lile na hususan katika kuboresha mifugo yetu na huduma nyingine. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved