Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 1 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 13 | 2022-11-01 |
Name
Ussi Salum Pondeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chumbuni
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: -
Je, ni kwa nini kusiwe na Mahakama ya Rufaa Tanzania Kanda ya Zanzibar badala ya kesi kusikilizwa kwa mwaka mara moja?
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Rufaa Kanda ya Zanzibar ipo kwa sasa na inaendesha shughuli zake kupitia Masijala ndogo iliyopo Jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar. Hata hivyo, Serikali inaona umuhimu wa kuwa na jengo la Mahakama ya Rufani Zanzibar na inaendelea kulifanyia kazi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved