Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zahor Mohamed Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwera
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: - Je, ni kwa nini kusiwe na Mahakama ya Rufaa Tanzania Kanda ya Zanzibar badala ya kesi kusikilizwa kwa mwaka mara moja?
Supplementary Question 1
MHE. ZAHOR MOHAMED HAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na naomba niongeze swali moja la ziada.
Wanasema justice delayed is a justice denied, naomba kumuuliza Mheshimiwa Waziri, je, Serikali iko tayari sasa kuongeza uharaka wa jambo hili kwa sababu wananchi wamekuwa wakipata matatizo kwa muda mrefu? Nakushukuru sana. (Makofi)
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, nipende kujibu swali la nyongeza la ndugu yangu pale Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli uharaka upo na kwa sababu ni sehemu ya mchakato wa kupatikana kwa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo hayo, naomba Mheshimiwa Mbunge atupe nafasi tu na muda wa kutosha na ataona kinachoendelea kwa sababu kimsingi Mahakama ya Tanzania iko kwenye mabadiliko makubwa sana katika uwekezaji wake, kwenye majengo ya kutolea huduma. Kwa hiyo hata hili ndio maana tumelitolea maelezo kwamba tunalifanyia kazi na kazi itakwenda kwa kasi sana. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved