Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 8 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 120 | 2022-11-09 |
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA K.n.y. MHE. SEIF K. GULAMALI aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Choma – Ziba – Nkinga hadi Puge?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika naomba kujibu swali la Mheshimiwa Seif Khamis Gulamali Mbunge wa Manonga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa Barabara ya Choma – Ziba – Nkinga hadi Puge yenye jumla ya kilometa 109.56 ambayo inapita katika maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Ndala na Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, Serikali kupitia Wakala wa Barabara nchini TANROAD, imeamua kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 kwa lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved