Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA K.n.y. MHE. SEIF K. GULAMALI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Choma – Ziba – Nkinga hadi Puge?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. SAMWEL X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Haidong - katesh imeshatengewa milkioni 300 kwa ajili ya ujenzi na milioni 280 kwa ajili ya usanifu wa kina. Je, Serikali ina mpango gani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pilli, Barabara ya Nangwa – Kondoa ina daraja ambalo limekuwa likikwamisha wananchi, daraja la Munguli, ilitengewa milioni 600. Je, ujenzi wake utaanza lini?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Xaday, Mbunge wa Hanang, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Hydom – Katesh ipo kwenye mpango na imepangiwa fedha. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa utekelezaji ni mwaka huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, Daraja la Munguli linalounganisha Kondoa na Hanang pia limetengewa fedha kwa ajili ya kulijenga Mwaka huu wa fedha. Ahsante.