Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 3 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 33 2023-04-06

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kufuta Hati ya Umiliki wa Shamba la Mwekezaji katika Kijiji cha Mawalla - Kilolo ambalo limetelekezwa?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, shamba lililotelekezwa katika Kijiji cha Mawalla, ni shamba lenye Hati Na.16633 lenye ukubwa wa ekari 639 ambalo linamilikiwa na Ndugu Mbaraka Mazrui. Mmiliki wa shamba hili alitelekeza shamba tangu mwaka 1980. Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Iringa, imelitambua shamba hili kama shamba lililotelekezwa.

Mheshimiwa Spika, kufuatia hali hiyo, Serikali imeanza hatua za awali za ubatilishaji wa shamba husika na pindi hatua hizo zitakapokamilika, mapendekezo yatawasilishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya ubatilishaji.