Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 3 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 37 | 2023-04-06 |
Name
Neema William Mgaya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itakamilisha Ujenzi wa Barabara ya Njombe – Ludewa – Itoni hadi Manda kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi kwa kiwango cha zege wa Barabara ya Itoni - Ludewa hadi Manda yenye urefu wa kilomita 211.42. Ujenzi kwa kiwango cha zege wa sehemu ya Lusitu – Mawengi kilomita 50 umekamilika na ujenzi wa sehemu ya Itoni – Lusitu kilomita 50 unaendelea.
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa sehemu zilizobaki utaendelea kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved