Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 80 2023-04-14

Name

Michael Mwita Kembaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza: -

Je, ni lini chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime TC kitaanza kufanya kazi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwita Kembaki Michael, Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Magena kilichopo Halmashauri ya Mji wa Tarime kimekwishakamilisha ujenzi wa Jengo la kuhifadhia maiti. Aidha, Halmashauri inaendelea na taratibu za ununuzi wa jokofu la kuhifadhia maiti baada ya kupokea fedha za ununuzi wa vifaatiba shilingi milioni 150 kutoka Serikali Kuu katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.