Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 7 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 87 2023-04-14

Name

Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza: -

Je, Serikali ipo tayari kufanya mapitio ya tathmini kwa wananchi wanaopisha mradi wa kuboresha Bonde la Mto Msimbazi?

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas, Mbunge wa Kinondoni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kufuatia malalamiko ya wananchi yaliyojitokeza kuhusu uthamini wa mali katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi, Serikali kupitia Wizara yangu na Ofisi ya Rais, TAMISEMI inaendelea kufanyia kazi malalamiko hayo kabla ya kuidhinishwa kwa taarifa za uthamini. Aidha, zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi litafanyika baada ya malalamiko hayo kupatiwa ufumbuzi.