Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 7 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 90 2023-04-14

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaweka taa za barabarani katika Mji wa Mpwapwa ili kuongeza usalama nyakati za usiku?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 350 kwa ajili ya kuweka taa za barabarani katika Mji wa Mpwapwa kwa urefu wa kilometa 2.5. Kazi za uwekaji wa taa umeanza na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2023, ahsante.