Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 8 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 103 2023-04-17

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza: -

Je, ni lini wananchi wa Kata ya Sitalike waliopisha ujenzi wa barabara ya Sitalike hadi Mpanda Hotel watalipwa fidia?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wananchi wa Kata ya Sitalike hadi Mpanda wanaodai fidia ni wale walio kwenye eneo la nyongeza la upana wa hifadhi ya barabara la kutoka mita
22.5 kwenda mita 30.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuwalipa fidia wananchi hawa, ahsante.