Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 8 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 107 2023-04-17

Name

Mansoor Shanif Jamal

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwimba

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. SHANIF J. MANSOOR aliuliza: -

Je, ni lini Chuo cha VETA Ngudu Kwimba kitakamilika?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shanif Jamal Mansoor, Mbunge wa Jimbo la Kwimba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kukamilisha ujenzi wa vyuo vya VETA Nchini. Kwa sasa inakamilisha hatua ya uwekaji wa samani pamoja na kuandaa rasilimaliwatu kwa lengo la kuviwezesha vyuo vya VETA ikiwemo Chuo cha Ngudu kuanza kutoa mafunzo kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Chuo cha VETA Ngudu upo katika hatua ya ukamilishaji na umefikia asilimia 97. Aidha, Wizara kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshapeleka kiasi cha shilingi 189,607,486.00 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa chuo hicho, nakushukuru.