Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 9 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 113 2023-04-18

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Primary Question

MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Babati Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa Barabara ya Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu, yenye urefu wa kilomita 50 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.