Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 10 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 123 2023-04-19

Name

Bonnah Ladislaus Kamoli

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Segerea

Primary Question

MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza: -

Je, ni Watanzania wangapi wamejitokeza na kupata fursa ya mafunzo maalum ya ujuzi yaliyotangazwa kupitia VETA kote nchini?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bonnah Ladislaus Kamoli, Mbunge wa Segerea kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tangu kuanza kutekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi mwaka 2016/2017, kupitia Vyuo vya VETA, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) na Vyuo Binafsi, jumla ya vijana walioomba mafunzo ni 215,233 na waliopatiwa mafunzo ya ujuzi ni 96,894 ambapo kati yao vijana 74,578 wamepatiwa mafunzo kwa njia ya uanagenzi na vijana 22,296 wamepatiwa mafunzo kupitia njia ya urasimishaji ujuzi (RPL).

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.