Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 10 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 127 2023-04-19

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaondoa makato yaliyopo kwenye Vyama vya Msingi kwa Wakulima wa Kahawa Mbozi?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Ranwell Mwenisongole, Mbunge wa Mbozi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na mapitio ya makato yaliyopo kwenye vyama vya ushirika kwa wakulima katika mazao mbalimbali ikiwemo zao la kahawa. Kufuatia malalamiko tuliyoyapokea kutoka kwa wakulima wa kahawa Mkoani Songwe, Serikali iliunda Timu kwa ajili ya kufuatilia na kufanya tathmini kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo zao la kahawa ikiwemo suala la makato.

Mheshimiwa Naibu Spika, Timu hiyo imekamilisha tathmini na inatarajia kuiwasilisha Wizarani mapema Mwezi ujao. Hivyo, baada ya kupitia taarifa hiyo ya tathmini, Serikali itachukua hatua stahiki.