Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 11 Works, Transport and Communication Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 141 2023-04-20

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Minara ya simu katika Kata za Kikolo, Mbangamao, Kitanda na Kagugu - Mbinga?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kufikisha huduma ya mawasiliano nchi nzima. Aidha, kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali, Kata ya Kitanda imejumuishwa katika utekelezaji wa mradi huo ambapo utekelezaji wake umeanza.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kwa upande wa kata zilizowasilishwa kuwa na changamoto ya mawasiliano ambazo ni Kata za Kikolo, Mbangamao na Kagugu, zitafanyiwa tathmini na kuchukua hatua stahiki, ahsante.