Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 17 Policy, Coordination and Parliamentary Affairs Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge 212 2023-05-03

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza: -

Je, lini Serikali italigawa Jimbo la Kilindi?

Name

Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE NA URATIBU) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Hivyo, kwa kuzingatia taratibu na vigezo, muda wa kugawa majimbo utakapofika tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa mchakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa Kikatiba, ahsante.