Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 18 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 233 | 2023-05-04 |
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA Wilayani Kilombero baada ya wanachi kutenga eneo la hekari 30?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Ni azma ya Serikali kujenga chuo cha ufundi stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2203, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyuo vya VETA katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazijajengewa vyuo hivyo. Tayari Serikali imeshakamilisha kuandaa michoro na upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya ujenzi.
Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Kilombero eneo lililotengwa kujengwa chuo cha ufundi stadi ni katika Kijiji cha Nakaguru Kata ya Mchombe. Aidha, tayari kiasi cha shilingi million 45 kimetolewa mwezi Machi, 2023 kwa ajili ya shughuli za awali za ujenzi wa chuo hicho.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved