Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 21 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 273 2023-05-09

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Singida – Ilongero hadi Haydom?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abeid Ramadhani Ighondo, Mbunge wa Singida Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TANROADS tayari imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina pamoja na kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Singida – Ilongero – Haydom yenye urefu wa kilometa 93. Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi, ahsante.