Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 24 Works, Transport and Communication Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 311 2023-05-12

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA K.n.y. MHE. DEUS C. SANGU aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatatua changamoto za mawasiliano ya simu Kata za Milepa, Zimba, Kaengesa na Lusaka?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI, alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari napenda kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilibaini kuwepo kwa changamoto katika Kata za Lusaka, Milepa, Kaengesa pamoja na Zimba. Hata hivyo, Kata ya Lusaka imepata mtoa huduma wa kufikisha huduma za mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata za Milepa, Zimba pamoja na Kaengesa zitafikishiwa huduma za mawasiliano kulingana na upatikanaji wa fedha.