Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 1 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 19 2023-08-29

Name

Santiel Eric Kirumba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SANTIEL E. KIRUMBA aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kuhimiza mashirika mengine ya simu kujiunga na mpango wa M-Mama kwani umekuwa msaada kwa wajawazito wengi?

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Santiel Eric Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mfumo wa M-mama unatekelezwa na kusimamiwa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Vodacom, USAID, Vodafone Foundation, Pathfinder International na Touch Foundation. Mfumo huu unalenga kusaidia upatikanaji wa usafiri wa dharura kwa mama mjamzito, mama aliyejifungua na mtoto mchanga kote nchini.

Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo ya mfumo kwa haraka na kwa kuwafikia walengwa wengi zaidi, kuna haja ya wadau mbalimbali kuongeza nguvu kwa kushirikiana katika utekelezaji wakiwemo watoa huduma wengine wa mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, natumia fursa hii kuwaalika mashirika binafsi wakiwemo watoa huduma wengine wa mawasiliano pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wajitokeze kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa Mfumo wa M-mama hapa nchini.