Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 3 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 44 | 2023-08-31 |
Name
Charles Muguta Kajege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji Kata za Kisorya, Igundu, Kwiramba, Namuhura, Butimba na Kasuguti - Mwibara?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Charles Muguta Kajege, Mbunge wa Mwibara, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na zoezi la kubaini maeneo yote yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji nchini ili kuyapima na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kupata sgharama halisi za kutekeleza miradi hii kabla ya kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Tume imejipanga kuyafikia maeneo mbalimbali yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji nchini ikiwemo maeneo yanayofaa kwa umwagiliaji yaliyopo ndani ya Jimbo la Mwibara ili kuingiza kwenye mpango wa utekelezaji, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved