Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 5 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 61 | 2023-09-04 |
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: -
Je, Serikali haioni haja ya kuharakisha uwekaji samani kwenye maktaba na maabara Chuo cha FETA Mikindani?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Agnes Elias Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024 Serikali kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia katika Kampasi zake ikiwemo ujenzi wa maabara na maktaba katika kampasi ya Mikindani. Pindi tuu ujenzi wa majengo hayo ya maktaba na maabara yatakapokamilika katika kampasi ya Mikindani, Serikali itaweka samani kwenye miundombinu hiyo muhimu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved