Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuharakisha uwekaji samani kwenye maktaba na maabara Chuo cha FETA Mikindani?
Supplementary Question 1
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili madogo nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, sasa ni mwaka wa tano tangu 2018 maktaba ilipokamilika, thamani zake ziko wapi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, maabara ilipanga kukamilika Oktoba, 2022 na kwa sasa imefikia asilimia 35, nini tamko la Serikali?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwamba Wizara ilikuwa inasubiri ukamilishaji wa maktaba na maabara na baada na ukamilishaji huo, Serikali inakwenda kuweka samani zote. Kwa kuwa tayari maktaba imeshakamilika, bado maabara, Wizara ilikuwa inasubiri vyote vikamilike kwa pamoja ili samani hizo zote ziende kwa pamoja. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge avute Subira, jambo hili tunalifuatilia. Leo jioni tukutane mimi na yeye twende pale Wizarani tufuatilie tuone jambo hili linafika mwisho kwa kiwango hiki, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved