Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 7 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 99 2023-09-06

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:-

Je, nini mpango wa kuhakikisha Majukwaa ya Kuwezesha Wanawake Kiuchumi yanaleta tija kwenye mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Elias Mahawanga, Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi yameleta tija kwenye asilimia 10 ya Halmashauri ya kuwezesha kuunda vikundi vya kiuchumi ambavyo hukutanisha wanawake katika ngazi zote za jamii ili kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi hususan biashara, kilimo, madini, ujenzi, uchukuzi, usindikaji wa maliasili na mazao ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika jamii, ahsante.