Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 35 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 458 2023-05-29

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha kuwa wakulima wa korosho wanapata mikopo nafuu ili waweze kugharamia kilimo hicho?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania inaratibu uwezeshaji wa wakulima wa korosho kupata mikopo ya kuendeleza zao la korosho ikiwemo pembejeo na utunzaji wa mashamba. Uwezeshwaji huo utafanyika kupitia Vyama Vikuu vya Ushirika kuwawekea dhamana wakulima ili waweze kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kuwaunganisha wakulima na taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu kuanzia asilimia tisa kushuka chini.