Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 44 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 567 2023-06-09

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: -

Je, kwa nini Serikali haipeleki fedha za maendeleo kwa wakati katika Halmashauri nchini?

Name

Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Grace Victor Tendega, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikipeleka fedha kwa wakati, mfano hadi kufikia mwezi Mei, 2023 kiasi cha shilingi trilioni 1.08 sawa na 116% zilipelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kote.

Mheshimiwa Spika, miradi inayotekelezwa na wakandarasi fedha hutolewa kulingana na hati ya madai ya kazi kulingana na utekelezaji wa majukumu hayo. Aidha, kwa miradi Iinayofanywa na force account, fedha hutolewa kwa kuzingatia utayari wa Halmashauri wa kuanza utekelezaji wa miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, ufafanuzi wa taratibu hizi unatolewa kulingana kwa mujibu wa kanuni na mwongozo wa utoaji fedha katika utekelezaji wa bajeti za Serikali ya mwaka 2021 iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango.