Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: - Je, kwa nini Serikali haipeleki fedha za maendeleo kwa wakati katika Halmashauri nchini?

Supplementary Question 1

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwanza nishukuru kwa majibu, lakini Serikali imesema itasimamia mikoa ili iweze kusimamia Halmashauri zisizo na utayari wa kuanza kutekeleza miradi.

Mheshimiwa Spika, lakini mikoa yenyewe imekuwa na chagamoto ya kuwa na fedha ambazo zinafanya ufatiliaji, tumekuwa tukiona tukienda ndio tunakwenda nao.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwawezesha kifedha Sekretarieti za Mikoa ili zitekeleze wajibu wao ipasavyo?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; fedha hizi hutolewa chini ya masharti ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982; zipo Halmashauri zinapata fedha zaidi ya walichoomba na ziko Halmashauri zinapata pungufu ya walichoomba na zipo zinazocheleweshewa kabisa kupata kuanzia mwezi wa tano hadi wa sita, na Halmashauri zinazopata zaidi zinafanya ubadhirifu wa kutumia fedha zaidi nje ya matumizi ambayo walipanga na nyingine zinazopata kidogo hazitekelezi mikakati yao kikamilifu. (Makofi)

Je, Serikali ina mkakati gani na kauli gani tunaipata kutoka kwa Serikali kuhusu suala hili? Ahsante.

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Grace Victor Tendega kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na fedha zinazotakiwa kupelekwa katika mikoa nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, fedha zote zinazopelekwa katika maeneo yote kwa mujibu wa kanuni ambayo yeye mwenyewe ameiā€“cite inayotoa miongozo ya fedha, inataka wahusika waombe fedha TAMISEMI ili wapelekewe na kama yako maeneo ambayo yametokea mapungufu hayo nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tutafatilia na tungeomba taarifa hizo utupe za kina ili tuweze kuzifatilia.

Pili juu ya upendeleo; nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali haifanyi upemndeleo na kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi, miradi inayotekelezwa ndio ambayo inaielekeza Serikali ifanyeje, katika force account kinachofanyika ni kwamba Halmashauri husika inapokuwa tayari kutekeleza mradi inatoa taarifa kwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, na fedha zinapelekwa na katika ilani ambayo inasimamiwa na wakandarasi Serikali inachofanya ni kwamba baada ya mkandarasi ku-raise certificate basi Serikali inapeleka pesa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka nikuhakikishie na Bunge lako kwamba Serikali iko makini inaendelea kufanya kazi vizuri na kama yako mapungufu katika maeneo ambayo wewe Mheshimiwa Mbunge umewahi kupita, basi utupe taarifa tuweze kufatilia na kuyafanyia kazi. (Makofi)