Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 44 Works and Transport Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 579 2023-06-09

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa njia nne kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Kilwa kipande cha Mbagala Rangi Tatu hadi Kongowe utakamilika?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kuanza ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Mbagala Rangi Tatu hadi Kongowe, kilometa 3.8 katika mwaka wa fedha 2023/2024, ahsante.