Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 47 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 602 2023-06-13

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. JUDITH S. KAPINGA aliuliza:-

Je, kuna mkakati gani kuhakikisha uwepo wa walimu wa kutosha wa masomo ya hesabu na fizikia katika elimu msingi hadi kidato cha tano na sita?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI), alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Judith Salvio Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuajiri walimu wapya wa masomo ya sayansi ili kukabiliana na upungufu uliopo ambapo kwa mwaka 2022/2023, tayari walimu 13,130 wameshapangiwa vituo vya kazi wakiwemo walimu wa masomo ya hesabu na fizikia.