Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 47 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 610 2023-06-13

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa Umwagiliaji wa Kisawasawa – Kilombero?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, skimu ya umwagiliaji Kisawasawa ipo katika Kata ya Kisawasawa, Tarafa ya Mang’ula Wilaya ya Kilombero. Skimu hiyo ipo umbali wa kilometa 43 kutoka Mji wa Ifakara kupitia barabara ya Ifakara - Mikumi. Skimu ya Kisawasawa ina eneo linalofaa kwa umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta 500.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetenga fedha za kwa ajili ya kufanya mapitio ya usanifu ili kupata gharama halisi za uendelezaji wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo.