Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 47 Finance and Planning Wizara ya Fedha na Mipango 612 2023-06-13

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Forodha cha Manyovu?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kavejuru Eliadory Felix, Mbunge wa Buhigwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa kituo cha huduma za pamoja mpakani (One Stop Boarder Post) cha Manyovu kilichopo Mkoani Kigoma na ujenzi upo kwenye taratibu za awali za kumpata mkandarasi, ahsante.